1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Germany yaanza kutekeleza mageuzi ya sheria ya uraia

27 Juni 2024

Sheria ya uraia iliyozua mjadala mrefu imeanza kutekelezwa Alhamisi nchini Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4hZbm
Hivi sasa watu wanaweza kuomba uraia baada ya kuishi Ujerumani kwa miaka mitano
Hivi sasa watu wanaweza kuomba uraia baada ya kuishi Ujerumani kwa miaka mitanoPicha: Fabian Sommer/dpa/picture alliance

Sheria hiyo mpya imerahisishia watu kupata pasi ya Ujerumani na uraia wa nchi mbili.

Hivi sasa watu wanaweza kuomba uraia baada ya kuishi Ujerumani kwa miaka mitano, tofauti na miaka minane ya huko nyuma, ikiwa tu watakuwa wanatimiza masharti.

Watoto waliozaliwa Ujerumani na wazazi wa mataifa mengine pia watapewa uraia wa Ujerumani ikiwa mzazi mmoja alikuwa ni mkaazi halali wa Ujerumani kwa miaka mitano badala ya minane.

Na hata Wajerumani wanaotaka uraia wa mataifa mengine hawatalazimika kupewa ruhusa maalumu kutoka mamlaka za Ujerumani.