1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yahitimisha shughui za kijeshi Niger

Angela Mdungu
31 Agosti 2024

Wanajeshi wa mwisho wa Ujerumani waliokuwa Niger, wameondoka nchini humo na kurejea nyumbani. Maafisa wa jeshi wa mataifa hayo mawili walitoa taarifa ya pamoja ya kuhitimisha shughuli za jeshi hilo Ijumaa jioni.

https://p.dw.com/p/4k8ON
Niger
Wanajeshi wa mwisho wa Ujerumani wameondoka NigerPicha: Gazali Abdou Tasawa/DW

Wanajeshi hao walisalia Niger baada ya Ujerumani na nchi hiyo iliyo chini ya utawala wa Kijeshi kufanya makubaliano ya muda yaliyowaruhusu kuendelea kuendesha kambi yao mjini Niamey hadi mwishoni mwa mwezi Agosti.

Soma zaidi: Yafahamu mataifa mengine ya magharibi yenye vikosi vya kijeshi Afrika Magharibi

Vikosi vya Ujerumani vilikuwa vikiendesha shughuli zake katika kambi hiyo tangu Februari 2016 ikiwa na wafanyakazi 3,200. Tangu utawala wa kijeshi ulipoingia madarakani Niger Julai 2023, taifa hilo limekuwa na uhusiano mbaya na washirika wake wa magharibi zikiwemo Ufaransa na Marekani.