Ujerumani yainyuka Bosnia 2-1
12 Oktoba 2024Matangazo
Timu ya taifa ya Ujerumani imeilaza Bosnia na Herzegovina 2-1 na kuisogelea robo fainali ya Ligi ya Mataifa Ulaya usiku wa kuamkia Jumamosi.
Katika dakika ya 30 ya mchezo, mchezaji wa Bayer Leverkusen,Florian Wirtz alitoa pasi kwa Denis Undav na kutia wavuni goli la kwanza, dakika 6 baadaye Undev alifunga goli la pili na kuwainua tena wajerumani. Zikiwa zimesalia dakika 20 mpira kumalizika Bosnia walipata goli la kufutia machozi kupitia kwa nyota wao Edin Dzeko.
Soma zaidi. Ujerumani yaanza maisha vizuri bila ya Toni Kroos na Neuer
Ushindi huo unaifanya Ujerumani kufikisha alama saba baada ya kucheza mechi tatu, alama mbili mbele ya Uholanzi iliyotoa sare ya 1-1 dhidi ya Hungary na ambayo watacheza nayo siku ya Jumatatu mjini Munich.