Ujerumani yakanusha Israel imefanya mauaji ya halaiki Gaza
6 Desemba 2024Alipoulizwa maoni yake kuhusu ripoti hiyo ya Amnesty International, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani Sebastian Fischer amewaambia waandishi wa habari kuwa, haamini kwamba kulikuwepo nia ya kutokomeza jamii nzima ya Wapalestina.
Hata hivyo, msemaji huo ameeleza kuwa wanazichukulia tuhuma zilizotajwa ndani ya ripoti hiyo kwa uzito mkubwa na kwamba wanaendelea kuzichambua.
Amnesty International yaishtumu Israel kwa mauaji ya halaiki katika ukanda wa Gaza
Amnesty International ilichapisha ripoti yenye kurasa 300 kuhusu mashambulizi ya Israel katika ukanda Gaza, ikisema ripoti hiyo ilizingatia uchunguzi wa picha za setilaiti na ripoti za moja kwa moja za wakaazi wa Gaza.
Israel hata hivyo imekanusha ripoti hiyo na kuitaja “kama uongo mtupu.”