Ujerumani yaridhia rasimu ya kuwarudisha watu kwao
25 Oktoba 2023Matangazo
Lengo kuu la muswada huo uliowasilishwa na waziri wa Masuala ya Ndani Nancy Faeser, ni kupunguza idadi ya juhudi zinazofeli dakika za mwisho za kuwarudisha watu makwao.
Muswada huo unarefusha muda ambao mtu anaweza kuwekwa kizuizini kabla ya kurudishwa kwao kutoka siku 10 hadi siku 28.
Soma pia:Utafiti: Ubaguzi dhidi ya watu weusi bado upo Ulaya
Rasimu hiyo pia inaweka sheria kali dhidi ya wasafirishaji watu kinyume cha sheria na upanuzi wa mamlaka za maafisa.
Chini ya sheria hiyo mpya, maafisa wataruhusiwa kuingia katika majumba ya watu kuwasaka wale wanaopaswa kurudishwa makwao.