Ujerumani yazidi kushinikizwa kuisaidia Ukraine
20 Januari 2023Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine na viongozi wengine wameikosoa serikali ya Ujerumani kwa kujizuia kuipatia silaha nzitonzito za ziada Ukraine. Hii leo serikali ya Ujerumani na waziri wake mpya wa ulinzi Boris Pistorius watakabiliana na mtihani wao mkubwa wa kwanza katika mkutano na maafisa wa ngazi za juu wa Marekani.Akizungumzia yatakayojadiliwa leo waziri wa ulinzi wa Ujerumani amesisitiza Marekani ni mshirika muhimu wa Ujerumani. Pistorius atakutana na waziri mwenzake wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin katika kambi ya kijeshi ya Marekani ya Ramstein hapa Ujerumani kujadili suala la kuipelekea silaha zaidi Ukraine. Pistorius jana aliweka wazi kwamba nchi yake itachukua hatua kwa ushirikiano na Marekani. Marekani inaiunga mkono Ujerumani.