1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe wa ECOWAS wawasili Sierra Leone kujadili usalama

Hawa Bihoga
24 Desemba 2023

Ujumbe wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS ukiongozwa na viongozi wa Senegal na Ghana umewasili nchini Sierra Leone ili kuweka msingi wa "kuimarisha usalama" baada ya jaribio la mapinduzi.

https://p.dw.com/p/4aXYo
Usalama  | Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio
Rais wa Sierra Leone Julius Maada BioPicha: Phil Noble/REUTERS

Taarifa zinasema kwamba Rais wa Senegal Macky Sall na Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo wote wako mjini Freetown kujadili hali ya usalama na Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Sierra Leone Timothy Kabba ameeleza katika mahojiano ya redio kwamba baada ya jaribio la kutaka kuipindua serikali iliochaguliwa kidemokrasia, ECOWAS ilizingatia suala la usalama na kuamua kutuma ujumbe wa kuleta utulivu nchini Sierra Leone.

Soma pia:Sierra Leone: Shambulio la Jumapili ni jaribio la mapinduzi

Mnamo Novemba 26, watu waliokuwa na silaha walivamia ghala la silaha la kijeshi, kambi mbili, magereza mawili na vituo viwili vya polisi, wakipambana na vikosi vya usalama ambapo watu 21 waliuwawa na wafungwa kutoroka kabla ya mamlaka kudhiditi hali.