1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Ukanda wa Gaza kwazidi kutokota

10 Mei 2023

Jeshi la Israel na wanamgambo katika Ukanda wa Gaza wamerushiana makombora leo katika ongezeko baya zaidi la machafuko katika ukanda huo wa pwani wa Palestina katika miezi kadhaa.

https://p.dw.com/p/4RA3R
Maroketi yamevurumishwa kutoka ukanda wa Gaza kuelekea Israel, Jumatano, Mei 10, 2023
Wanamgambo wa Palestina waliahidi kulipiza kisasi dhidi ya shambulizi la Israel lililowaua Wapalestina 16, ambao ni pamoja na maafisa watatu wa wanamgambo hao.Picha: Hatem Moussa/AP Photo/picture alliance

Israel ilitangaza kuwa inayalenga maeneo ya kufyatulia makombora ya kundi la wanamgambo la Islamic Jihad. Wizara ya afya ya Gaza imesema watu wanne wameuawa, siku moja baada ya mashambulizi ya Israel katika maeneo ya Kipalestina kuwauwa watu 15. Mfumo wa ulinzi wa makombora ya angani wa Israel umeripotiwa kuyaharibu makombora katika anga za mji wa pwani wa Ashkelon na kwingineko katika upande wa kusini. Jeshi la Israel limesema leo kuwa mashambulizi yake yaliwalenga wanamgambo waliokuwa njiani kwenda katika eneo la kufyatulia makombora katika mji wa Khan Yunis kusini mwa Gaza. Kundi la Islamic Jihad liliapa jana kulipiza kisasi, huku Israel ikiwaonya wakaazi wake karibu na mpaka huo kujificha katika mahandaki ya kujikinga na mabomu.