1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukimwi - Kujikinga dhidi ya gonjwa hili

14 Januari 2009

Licha taarifa kuhusu viwango vya maambukizi ya virusi vya HIV kupungua hapa na pale barani Afrika, bado viwango hivyo ni vya juu sana kuliko sehemu yoyote nyingine duniani.

https://p.dw.com/p/DnAv
Picha: laif

Kiasi cha asilimia 70 ya watu wote walioambukizwa virusi va ukimwi duniani kote wanaishi Afrika. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, kiasi cha Waafrika milioni mbili wanaambukizwa virusi hivyo kila mwaka. Kampeni za kuielimisha jamii zinafanyika katika nchi kadhaa, lakini dhana zisizofaa kuhusu virusi vya HIV na ukimwi bado zinaendelea kuwapo. Kwa mfano, baadhi ya wanaume bado wanasisitiza kuwa wanaweza kujikinga kwa kuoga maji moto baada ya tendo la kujamiiana.

Wasi wasi wa kutengwa

Kuishi na hofu ya kuambukizwa virusi vya HIV bado ni changamoto kubwa. Watu wengi ambao ni waathirika wa virusi vya HIV wanaficha ukweli huu kwa sababu wanahofu ya kunyanyapaliwa na jamii inayowazunguka. Lakini maambukizi ya virusi vya HIV sio tena hukumu ya kifo: Dawa za kurefusha maisha zimesaidia wengi waliyoambukizwa virusi hivyo, kuishi maisha marefu na yenye mafanikio.

Moja kati ya malengo ya mradi huu wa „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ ni kuondoa hali ya kutokuwa na elimu juu ya virusi vya HIV na kimwi. Vipindi vyetu vinaangalia hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV na jinsi ya kujikinga. Vipindi hivi vitatoa kwa wasikilizaji wake taarifa za kina juu ya vipi muathirika anaweza kuishi na virusi vya HIV na jinsi ya kuishi na watu ambao wameathirika. Lakini mtu yeyote ambaye anatarajia kupata masomo ya kinadharia tu, atashangaa kwani „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ inatoa taarifa na pia kuburudisha.

Kwa taarifa zaidi ama kusikiliza vipindi, tafadhali tembelea tovuti yetu : www.dw-world.de/lbe „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ kinadhaminiwa na wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani.