1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ursula: Ukraine itaamuwa juu ya mahusiano ya China na EU

30 Machi 2023

Mkuu wa Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen ameionya Beijing kuwa msimamo wake kuhusu vita vya Urusi nchini Ukraine utaamua jinsi yatakavyokuwa mahusiano ya China na Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/4PWCD
Ursula von der Leyen / Rede 30.03.2023
Picha: VALERIA MONGELLI/AFP/Getty Images

Hata hivyo amesema kuwa Ulaya haitaki kutengana na China. Akizungumza mjini Brussels, von der Leyen amesema ni wazi kuwa china, chini ya Xi inaanza kuwa kandamizi zaidi ndani ya nchi na yenye uthubutu zaidi nje ya nchi.

Rais huyo wa Halmashauri Kuu ya Ulaya ataandamana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwenda Beijing wiki ijayo huku viongozi wa Ulaya wakilenga kufanya mashauriano na Rais wa China Xi Jinping.