MigogoroUkraine
Ukraine kuomba idhini pana ya kushambulia ndani ya Urusi
3 Juni 2024Matangazo
Hiyo ni baada ya Marekani kuondoa kwa kiasi vikwazo vya matumizi ya baadhi ya silaha zinazotolewa na nchi za Magharibi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari sambamba na Waziri mwenzake wa Estonia kwamba, bado hawajaruhusiwa kwa asilimia 100 na ruhusa hiyo inatolewa kwa masharti yanayotakiwa kuzingatiwa.
Amesema wataendelea kushirikiana na washirika wao wa magharibi juu ya uwezekano wa kuongeza matumizi ya silaha hizo.
Wiki iliyopita, Washington iliipa ruhusa Ukraine kutumia silaha inazopewa na magharibi kushambulia baadhi ya maeneo za kijeshi ndani ya Urusi kama sehemu ya juhudi zake za kukabiliana na mashambulizi ya Urusi katika jimbo la Kharkiv.