1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUjerumani

Ukraine yakanusha kuhusika na milipuko ya Nordstream II

15 Agosti 2024

Mshauri wa rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak, amekanusha kuhusika kwa nchi yake katika milipuko iliyosababisha kuharibiwa kwa bomba la gesi la Nord Stream 2.

https://p.dw.com/p/4jUSj
Ukraine yakanusha kuhusika na milipuko ya mabomba ya Nordstream
Ukraine yakanusha kuhusika na milipuko ya mabomba ya NordstreamPicha: Jens Büttner/dpa/picture alliance

Msemaji huyo wa rais amedai kwamba kitendo hicho kinaweza kufanywa tu na nchi yenye rasilimali na uwezo mkubwa wa kifedha na Urusi ndiyo iliyokuwa katika nafasi hiyo, kwa wakati huo.

Matamshi ya Podolyak yametolewa wakati ambapo Urusi imeanza kuwaondoa maelfu zaidi ya raia wake kutoka maeneo ya mpakani, baada ya Ukraine kusema kwamba inazidi kusonga ndani na uvamizi wake katika eneo la Kursk, kwa lengo la kuilazimisha Urusi kupunguza kasi yake ya mashambulizi.

Uvamizi uliofanywa na vikosi vya Ukraine kuanzia Agosti 6 nchini Urusi ndio uvamizi mkubwa kufanywa na nchi ya kigeni katika eneo huru la nchi hiyo tangu Vita vya Pili vya Dunia. Uvamizi huu umesababisha aibu kwa maafisa waandamizi wa jeshi la Urusi.