1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yasema wanajeshi wengi wa Korea Kaskazini wameuawa

18 Desemba 2024

Shirika la ujasusi la Ukraine limesema leo kuwa vikosi vya Korea Kaskazini vinavyolisaidia jeshi la Urusi kulikomboa eneo la Kursk linalokaliwa na Ukraine vimepoteza wanajeshi wake wengi.

https://p.dw.com/p/4oJhE
USA New York 2024 | Ukrainischer Präsident Selenskyj spricht vor UN-Generalversammlung
Picha: Mike Segar/REUTERS

Kwa mujibu wa mazungumzo ya simu yaliyorekodiwa kwa njia ya siri, shirika la ujasusi la Ukraine SBU limeeleza kuwa zaidi ya askari 200 wa Korea Kaskazini waliojeruhiwa wamelazwa hospitali karibu na mji mkuu Moscow.

Hata hivyo taarifa hizo za SBU hazikuweza kuthibitishwa kwa njia huru.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky pia amegusia mara kadhaa kuhusu kuuliwa wanajeshi wa Korea Kaskazini katika siku za hivi karibuni.

Zelensky pia ameishtumu Urusi kwa kuchoma maiti za wanajeshi waliouawa vitani ili kuficha idadi kamili ya vifo.