Ukraine yasonga mbele na mpango wake wa amani
14 Januari 2024Ukraine inasonga mbele na mpango wake wa amani kwa lengo la kuvimaliza vita na Urusi vya karibu miaka miwili sasa. Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa aahidi kuiunga mkono Ukraine
Mpango huo utajadiliwa kwenye mkutano wa maafisa wa usalama wa taifa, kutoka duniani kote unaofanyika kwenye kitongoji cha burudani cha Davos nchini Uswisi.Zelenskiy asema usitishaji mapigano Ukraine utainufaisha tu Urusi
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, aliyepangiwa kuhutubia kongamano la kiuchumi la Dunia (WEF) huko Davos hakuwapo kwenye kikao cha ufunguzi leo asubuhi, kilichowaleta pamoja washiriki zaidi ya 80 kutoka nchi na mashirika ya kimataifa.
Zelensky aapa kulipiza mashambulizi yaliyofanywa na Urusi
Zelensky aliwakilishwa na mkuu wake wa watumishi Andriy Yermak kwenye kikao hicho kilichohudhuriwa pia na mwakilishi maalum wa Marekani, Penny Pritzker anayeshughulikia ufufuaji wa uchumi wa Ukraine.
Naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani, James O`Brien, anayeshughulikia masuala ya Ulaya na bara Asia, pia alihudhuria mkutano huo.