1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelenskiy apendekeza ulinzi wa NATO kustisha vita na Urusi

30 Novemba 2024

Ukraine inaweza kukubali kusitisha mapigano na Urusi iwapo NATO itaongeza ulinzi wake kwenye maeneo yanayodhibitiwa na Ukraine, Rais Volodymyr Zelensky alisema Ijumaa.

https://p.dw.com/p/4nb4k
DW Video | Wanajeshi wa Ukraine wakiwa kwenye sare.
Wanajeshi wa Ukraine wakifanya mazoezi ya kulenga shabaha.Picha: Rosie Birchard/DW

Vikosi vipya vya Ukraine vinapelekwa tena kwenye maeneo ya mstari wa mbele yanayokabiliwa na kitisho kikubwa ya Pokrovsk na Kurakhove, ili kukabiliana namajeshi ya Urusi yanayosonga mbele, huku Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, akipendekeza kusitisha mapigano iwapo NATO itachukua hatua ya kulinda maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa Ukraine.

Soma pia: Biden aandaa msaada wa silaha wa dola mil. 725 kwa Ukraine

Katika mapambano makali katika mkoa wa Donbass, vikosi vya Ukraine vinajaribu kuzuia Urusi isisogee kuelekea miji muhimu kama Dnipro na Zaporizhzhya. Katika upande wa kidiplomasia, Zelensky amesema Ukraine inaweza kukubali usitishaji vita na Urusi, ikiwa NATO itatoa ulinzi kwa maeneo ya nchi yanayodhibitiwa na Ukraine.

Wakati huo, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amemhakikishia Zelenskiy mshikamano wa Ujerumani katika mazungumzo kwa njia ya simu, ambamo pia alimuarifu kuhusu mazungumzo yake ya Rais wa Urusi, Vladmir Putin.