Ukuaji wa uchumi ulimwenguni kupungua mwaka 2023
26 Januari 2023Matangazo
Idara ya masuala ya uchumi na masuala ya kijamii ya Umoja wa Mataifa imesema kasi ya ukuaji wa uchumi kwa sasa ulimwenguni imepungua kuanzia mataifa yanayoendelea hadi yaliyoendelea, huku mengi yakikabiliwa na kitisho cha mdororo wa uchumi kwa mwaka huu wa 2023.
Ripoti ya Umoja huo ya kurasa 178 aidha imesema makisio ya ukuaji kwa mwaka huu ya asilimia 1.9, tofauti na asilimia 3 iliyokadiriwa mwaka 2022, ni ya chini mno kushuhudiwa katika miongo ya karibuni.
Hata hivyo imekisia ukuaji wa wastani wa hadi asilimia 2.7 mwaka 2024 ikiwa mfumuko wa bei na mtikisiko wa kiuchumi vitapungua.