Ulaya ya Kati yakumbwa na mafuriko
7 Agosti 2023Mataifa yaliyoathirika zaidi ni Slovenia, Austria na Croatia ambako kwa jumla vifo vya watu sita vimeripotiwa wakiwemo raia wawili wa Uholanzi waliopigwa na radi wakiwa matembezi nchini Slovenia.
Waziri Mkuu wa Slovenia Robert Golob amekadiria kuwa hasara iliyotokana na mafuriko hayo imefikia Euro milioni 500 na ameomba msaada wa haraka kutoka Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Kujihami ya NATO.
Soma zaidi: Ukraine yasema huenda mazungumzo ya amani kati yake na Urusi yakasambaratika kabisa
Kingo za mito mikubwa mitatu nchini humo zimepasuka na baadhi ya vijiji, barabara na njia za reli zimefunikwa na maji.
Nchini Austria, zaidi ya maporokomo 80 ya udongo yameripotiwa wakati kwenye taifa jirani la Croatia hali ya tahadhari imetangazwa katika baadhi ya majimbo kutokana na kitisho cha kutokea maafa kutokana na mvua zinaendelea kunyesha.