1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Ulaya yawawekea vikwazo maafisa 6 wa kijeshi wa Sudan

24 Juni 2024

Mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya hii leo wameidhinisha vikwazo dhidi ya watu sita wa Sudan wanaohusishwa na vita kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF iliyoligubika taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4hRY6
Sudan| Darfur | El Fasher | vita vya wenyewe kwa wenyewe
Sudan imetumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu Aprili 15,2023. Picha: AFP

Orodha hiyo inamjumuisha jenerali wa kijeshi wa RSF wa Darfur Magharibi ambaye kulingana na Baraza la Umoja wa Ulaya anawajibika kwa mauaji ya kiholela, kuchochea mauaji ya kikabila, uhalifu wa kingono, uporaji na kuchoma nyumba za watu.

Kwenye orodha hiyo pia yumo mshauri wa masuala ya fedha wa RSF pamoja na kiongozi mashuhuri wa ukoo wa Mahamid mwenye mahusiano na RSF huko Darfur Magharibi.

Kwenye upande wa jeshi, vikwazo hivyo vimemkumba mkurugenzi wa shirika kubwa la vifaa vya jeshi, DIS na kamanda wa jeshi la anga wakihusishwa na mashambulizi holela ya anga kwenye maeneo yanayokaliwa na watu wengi.