1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiPakistan

Sehemu kubwa Pakistan yakosa umeme

23 Januari 2023

Sehemu kubwa ya nchini Pakistan imekosa huduma za umeme kwa saa kadhaa Jumatatu asubuhi baada ya hatua ya serikali kuhifadhi nishati kugonga mwamba.

https://p.dw.com/p/4MbDD
Pakistan Sindh Tharparkar Frauen arbeiten an Solarenergieanlage
Picha: Afifa Nasarullah/DW

Kukatika huko kwa umeme kulizusha hofu na kuibua maswali kuhusu jinsi serikali inayokumbwa na ukata wa fedha inavyoushughulikia mgogoro wa kiuchumi wa nchi hiyo. 

Waziri wa Nishati wa Pakistan, Khurram Dastgir amesema kuwa wahandisi wanajitahidi kurejesha huduma za umeme kote nchini humo ukiwemo mji mkuu, Islamabad.

Aidha, amelihakikishia taifa kuwa umeme utarejeshwa kikamilifu katika muda wa saa 12 zijazo.

Kukosekana kwa umeme kuliwaacha watu wengi bila ya maji ya kunywa kwa sababu pampu za maji zinatumia umeme. Shule, hospitali, viwanda na maduka yalikosa umeme wakati huu wa msimu wa baridi kali.