Umoja wa Afrika
2 Februari 2009Matangazo
ADDIS ABABA.
Mkutano wa kilele wa nchi za Umoja wa Afrika unaendelea mjini Addis Ababa lakini ni viongozi 20 tu walioshiriki kwenye kikao cha kwanza kilichofanyika kwa faragha.
Habari zinasema nchi za Afrika zitaanza kutafakari njia za kuelekea kwenye kuunda serikali moja barani Afrika.
Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema viongozi kwenye mkutano huo wa Addis Ababa wamekubaliana kuunda mamlaka mpya ya Umoja wa Afrika, itakayochukua nafasi ya tume ya sasa ya Umoja huo. Akifafanua juu ya hatua hiyo, mwenyekiti wa tume hiyo Jean Ping amesema kuwa lengo la taasisi hiyo mpya ni kuunda serikali ya umoja kwa bara lote la Afrika.