SiasaLibya
Umoja wa Mataifa kuimarisha mazungumzo kuhusu uchaguzi Libya
20 Juni 2023Matangazo
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Libya Abdoulaye Bathily amesema anapanga kuimarisha mashauriano na vyama vinavyohasimiana nchini humo kufikia makubaliano ya mwisho katika miezi ijayo kuhusu masuala nyeti yanayokwamisha uchaguzi ulioahirishwa.
Bathily amelitahadharisha baraza la usalama kwamba kurefusha mkwamo uliopo sasa huenda kukasababisha janga kwa Libya na majirani zake.
Pia alisema ni muhimu wanachama wa baraza la usalama wazishinikize zaidi pande zinazohasimiana, wazungumze kwa kauli moja na wachukue hatua kuwaondoa viongozi wanaovuruga mchakato wa kufikia mapatano.