Vifo vya wanaovuka Mediterania vyaongezeka.
13 Aprili 2023Idadi ya watu waliokufa wakivuka bahari ya Mediterenia wakikimbilia Ulaya imefikia viwango amabavyo havijaonekana tangu mwaka wa 2017 ripoti ya Umoja wa Kimataifa imeonyesha.
Watu 441 wamefariki miezi mitatu ya kwanza ya 2023 huku idadi kamili ikidhaniwa kuwa juu Zaidi kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji.
Zaidi ya vifo 20,000 vimeripotiwa tangu mwaka wa 2014. “Mgogoro wa kibinadamu unaondelea Medierenia ya kati hauwezi kuvumilika,” Antonio Vitorino mkuu wa shirika la kimataifa la uhamiaji alisema.
Shirika la kimataifa la uhamiaji limeyalaumu mataifa kadhaa yanayoizunguka bahari hiyo bila kuyataja.Shirika hilo limekosoa kuchelewa kwa mataifa hayo kuanzisha shuguli za kutafuta na kuwaokoa kujikokota huko kukuchangia kuchangia vifo vingi.
Kufifia kwa shuguli za mashirika yasiyokua ya kiserikali katika bahari hiyo kumelaumiwa kwa kuchangia vifo vingi.Sera zilizoanzisha na mataifa kadhaa zimezidi kudhoofisha shuguli za mashirika yasiyokua ya kiserikali kuwaokoa wakimbizi wengi.
Italia imeyazuilia mashua ya mashirika yasiyo kua ya kiserikali mara kwa mara kwa sababu tofauti.
Serikali ya siasa za mrengo wa kulia ya Italia imezidi kuzizuia mashua zinazowabeba wakimbizi.
Idadi ya watu wanao jaribu kuvuka bahari ya Mediterenia imepongezeka huku watu 32,000 wakiingia Italia tangu mwanzo wa mwaka ikilinganishwa na watu 8,000 kipindi sawa mwaka uliopita.