Umoja wa Mataifa waadhimisha miaka 75 ya walinda amani
26 Mei 2023Matangazo
Guterres ameyasema hayo katika maadhimisho ya miaka 75 ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa, tangu Umoja huo ulipolituma jeshi la kwanza la kulinda amani mwaka 1948.
Kwenye maadhimisho hayo, Guterres aliwaomba mamia ya maafisa na wanadiplomasia kukaa kimya ili kuwakumbuka walinda amani hao na baadae aliwakabidhi medali kwa niaba ya wahanga hao waliokufa katika mataifa 39, mnamo mwaka 2022.
Ulimwengu washindwa kuwalinda raia kwenye maeneo ya mizozo
Umoja huo aidha umetumia siku hii kuwaenzi walinda amani zaidi ya milioni 2 kutoka nchi 125 waliohudumu katika operesheni 71 tangu Baraza la Usalama lilipotuma waangalizi wa kwanza wa kijeshi kusimamia utekelezaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Waarabu.