1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

UN yaonya hatua za haraka kukabiliana na mzozo wa Sahel

Sylvia Mwehozi
8 Juni 2024

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka ili kuepusha raia zaidi kuyakimbia makazi yao katika kanda ya Sahel inayokabiliwa na mzozo mkubwa wa kibinadamu..

https://p.dw.com/p/4gosF
Wakimbizi wa Mali wakichota maji
Kambi ya kaskazini mwa Burkina Faso inayowahifadhi wakimbizi wa MaliPicha: Olympia de Maismont/AFP

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka ili kuepusha raia zaidi kuyakimbia makazi yao katika kanda ya Sahel barani Afrika iliyokumbwa na machafuko na kushuhudia mzozo mkubwa wa kibinadamu.

Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, limesema kuwa zaidi ya watu milioni 3.3 wamelazimika kuyakimbia makazi yao katika nchi za Burkina Faso, Mali na Niger katika kipindi cha miaka minne iliyopita kutokana na mzozo uliochochewa na mabadiliko ya tabia nchi.UNICEF yalaani ongezeko la ukatili dhidi ya watoto, Sahel

Kwa miaka kadhaa sasa, kanda ya Sahel imekumbwa pia na wimbi la ghasia za makundi ya kigaidi pamoja na mapinduzi kadhaa ya kijeshi.

UNHCR imesema inahitaji dola milioni 443.5 ili kukidhi mahitaji ya dharura ya kibinadamu katika nchi za Burkina Faso, Mali, Niger, Mauritania na mataifa yaliyopo kwenye eneo la Ghuba ya Guinea.