1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa wawekea vikwazo makamanda Guinea-Bissau

19 Mei 2012

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limewawekea marufuku ya kutosafiri nje ya Guinea Bissau viongozi watano walioshiriki mapinduzi ya kijeshi ya Aprili 12 mwaka huu nchini humo.

https://p.dw.com/p/14yaS
Wanajeshi Guinea BissauPicha: picture-alliance/dpa

Pamoja na hatua hiyo baraza hilo pia limetisha kupiga marufuku ya silaha sambamba na kiuchumi iwapo taifa hilo la pwani ya Afrika Magharibi halitarejea katika utawala wa kiraia.

Katika taarifa ya mataifa 15 wanachama wa baraza hilo , imetaka makamanda wa kijeshi kuchukua hatua za haraka kurejesha na kuheshimu utaratibu wa katiba, ikijumuisha uchaguzi wa kidemokrasia, kuhakikisha wanajeshi wote wanarejea makambini na makamanda wa juu wa jeshi kuachia nafasi zao za mamlaka.

Baraza hilo la usalama liliweka azimio la kuzuia kusafiri kwa kiongozi wa mapinduzi Jenerali Antonio Injali na Meja Jenerali Mamadu Ture, Jenerali Estavao Na Mena, Brigedia Jenerali Ibraima Camara na Luteni kanali Daba Naualna.

From (L to R) Senegal's President Macky Sall, Guinea's President Alpha Conde and Togo's President Faure Gnassingbe attend an Economic Community of West African States (ECOWAS) meeting to discuss the Mali crisis and Guinea-Bissau's coup in Abidjan April 26, 2012. REUTERS/Luc Gnago (IVORY COAST - Tags: POLITICS)
Ujumbe wa ECOWASPicha: Reuters

Baraza hilo la usalama limeongea kwamba kuna watu wengine kadha wataongezwa katika kikwazo hico. Vurugu nchini Guinea-Bissau zilitokea ikiwa zimebaki wiki kadhaa kufanyika kwa uchaguzi mkuu.

Aprili 12 wanajeshi walivamia nyumbani mgombea wa urais alie anaeng'ara pamoja na rais wa mpito wa taifa hilo na kuwakamata. Tangu wakati huo wanasiasa hao walilikimbia taifa hilo.

Kwa zaidi ya miaka 40 sasa kumbukumbu zinaonsha kuwa hakuna kiongozi wa Guinea-Bissau, ambalo taifa lililokuwa likitawaliwa na Ufaransa, aliyewahi kumaliza muhula wake wa uongozi.

Taifa hilo lilikuwa likikabiliwa na mapinduzi ya mara kwa mara pia linataja kama njia muhimu ya kupitishia madawa haramu ya kulevya kutoka Amerika ya Kusini kuelekea Ulaya.

Jitiahada za sasa za baraza la usalama la umoja wa mataifa zinachachua zile zilikuwa zimeanzishwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS.

Mwandishi: Sudi Mnette/APE
Mhariri: Sekione Kitojo