Umoja wa ulaya kuikopesha Ukraine Euro bilioni 35
22 Oktoba 2024Matangazo
Serikali ya Ukraine inahitaji msaada wa kifedha ili kuimarisha uchumi wake, kuandaa jeshi lake na kuhakikisha kuwa gridi yake ya umeme inafanya kazi hasa msimu huu wa baridi wakati vikosi vya Urusivikizidisha mashambulizi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Mkopo huo wa Umoja wa Ulaya ambao uliidhinishwa na wabunge wengi ni sehemu ya mpango mkubwa wa dola bilioni 50 uliokubaliwa na mataifa yenye nguvu ya G7 mwezi Juni kwa Ukraine. Mkopo huo wa hivi punde unakamilisha idadi ya takriban euro bilioni 120 za msaada ambazo nchi nwananchama za Umoja wa Ulaya zimetoa kwa Ukraine tangu uvamizi wa Urusi nchini humo mwaka 2022.