BiasharaKenya
Umoja wa Ulaya na Kenya zafikia makubaliano ya kibiashara
19 Juni 2023Matangazo
Mkataba huo wa Ushirikiano wa Kiuchumi (EPA) utaipatia Kenya fursa ya ufikiaji wa soko inalolitegemea zaidi la Umoja wa Ulaya bila ushuru, na hivyo kuagiza bidhaa kama majani ya chai, kahawa na asilimia 70 ya maua yake.
Mazungumzo kuhusu makubaliano hayo yamekamilika rasmi katika hafla iliyofanyika jijini Nairobi na kuhudhuriwa na Rais wa nchi hiyo William Ruto, na waziri wake wa Biashara Moses Kuria pamoja na Kamishna wa Biashara wa Umoja wa Ulaya, Valdis Dombrovskis.
Mwaka 2014 Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati huo ikijumuisha Kenya, Rwanda, Uganda, Burundi na Tanzania, zilifikia makubaliano ya kibiashara lakini ni Kenya pekee iliyofikia katika hatua za mwisho.
AFP