Umoja wa Ulaya wapendekeza mkakati wa kuimarisha ulinzi
5 Machi 2024Matangazo
Makamu wa rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Margrethe Vestager amesema muungano huo unapaswa kuchukua wajibu zaidi katika kushughulikia masuala yake ya ulinzi na kuendelea kujitolea kikamilifu kwa washirika wake wa Jumuiya ya kujihami NATO, zaidi ameongeza "Bajeti za ulinzi katika nchi zote wanachama zinapanda kwa kasi, hivyo tunapaswa kubadili njia tunayotumia. Kwa kuwa tunataka kuwekeza zaidi, tunapaswa kufanya uwekezaji bora zaidi, ambao kwa kiasi kikubwa unamaanisha kuwekeza pamoja na kuwekeza Ulaya." Miongoni mwa mikakati iliyoainishwa ni utoaji motisha kwa wazalishaji silaha wa ulaya, uwekezaji zaidi, uzalishaji wa haraka na kuorodhesha kwa pamoja kiwango cha silaha walicho nacho.