Sheria na HakiAsia
EU waikosoa Mongolia kwa kutomkamata Putin
4 Septemba 2024Matangazo
Msemaji wa Umoja wa Ulaya amesema katika taarifa kwamba umoja huo unasikitika kwamba Mongolia, nchi iliyoridhia mkataba wa Roma ulioiasisi mahakama ya ICC, haikutimiza majukumu yake chini ya mkataba wa kutekeleza waranti wa kukamatwa.
Wakati haya yakiarifiwa, Umoja wa Mataifa umezikumbusha nchi zilizosaini mkataba wa Roma kwamba lazima ziheshimu mikataba ya kimataifa baada ya Putin kukwepa kukamatwa wakati wa ziara yake nchini Mongolia.
Soma pia:Putin atoa mwaliko kwa Mongolia kuhudhuria mkutano wa BRICS
Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema mjini New York kwamba nchi zilizosaini mikataba ya kimataifa zina wajibu kuiheshimu na kuitekeleza, ingawa hakutaka kutoa kauli moja kwa moja kuhusu suala la Putin.