Umoja wa Ulaya yaahidi kuongeza uwekezaji nchini Kenya
22 Februari 2023Akizungumza Jumanne katika siku ya kwanza ya Jukwaa la Biashara kati ya Kenya na Umoja wa Ulaya mjini Nairobi, Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Kenya Henriette Geiger, alisema uwekezaji huo utazilenga sekta ambazo bado hazijaimarishwa.
Geiger amesema mikataba mipya itakayotiwa saini ni sehemu ya mkakati wa Umoja wa Ulaya wa kukusanya takribani dola bilioni 340 kusaidia sekta ya miundombinu ya umma na binafsi, kote ulimwenguni ifikapo mwaka 2027.
Miongoni mwa makubaliano yatakayofikiwa ni pamoja na ahadi ya mchango wa dola milioni 200 kuisaidia benki ya biashara na maendeleo inayoendeshwa kwa pamoja na mataifa kadhaa ya Afrika.
Benki hiyo imekuwa ikizisaidia kampuni za mataifa ya mashariki na kusini mwa Afrika zilizoathirika na vita vya Ukraine