UN, Iran zahimiza ushirikiano kukabili dhoruba za mchanga
9 Septemba 2023Katika hotuba kwa njia ya video kwa wawakilishi wa takriban mataifa 50 na mashirika 15 yanayohudhuria kongamano la kimataifa la kukabiliana na dhoruba za mchanga na vumbi nchini Iran, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amewahimiza washirika wa kongamano hilo kutumia muda wao mjini Tehran kujenga uhusiano, kuimarisha ushirikiano na kujitolea kwa hatua zinazoweza kutekelezwa.
Soma zaidi: Iraq yakumbwa tena na dhoruba kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa
Wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, rais wa Iran Ebrahim Raisi, alitoa wito kwa mataifa katika kanda hiyo kuanzisha mfuko wa kutafuta suluhu za pamoja, na amezilaumu nchi zilizoendelea kiviwanda kwa kusababisha matatizo mengi, kupuuzia masuala ya mazingira.
Kulingana na wataalamu wa hali ya hewa, dhoruba za mchanga na vumbi zinatarajiwa kuongezeka katika nchi zinazokabiliwa na hatari zaidi ya mabadiliko ya tabianchi.