1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Kuundwe mataifa mawili katika mzozo wa Israel-Hamas

29 Novemba 2023

UN yatoa wito wa kuundwa mataifa mawili katika mzozo wa Israel na Hamas ukisema kuwa Jerusalem unapaswa kutumika kama mji mkuu wa mataifa hayo mawili.

https://p.dw.com/p/4Zb23
Israel- Hamas | Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio GuterresPicha: Brendan McDermid/REUTERS


Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuendeleza jitihada za kupatikana suluhisho la mataifa mawili katika mzozo wa Wapalestina na Israel, ukisema kuwa Jerusalem unapaswa kutumika kama mji mkuu wa mataifa hayo mawili.

Akitoa hotuba iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa jijini Geneva Tatiana Valovaya, amesema sasa ni wakati wa kusonga mbele katika dhamira ya wazi, isiyo ya kurudi nyuma, kuelekea suluhisho la mataifa mawili, kwa msingi wa maazimio ya Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa.

Soma pia:Wapatanishi waeleza matumaini ya kurefushwa usitishaji mapigano kwa siku mbili zaidi

Ameongeza kuwa hii ina maana Israel na Palestina kuishi kama majirani kwa amani na usalama huku Jerusalem ikitumika kama mji mkuu wa mataifa hayo mawili.

Miito ya kuwepo madola mawili imeongezeka kufuatia vita vya sasa kati ya Israel na wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas.