UN kuwaadhibu watakaobainika kuhusika na "ugaidi"
28 Januari 2024Guterres ameyasema hayo baada ya kuibuka kwa tuhuma kuwa, wafanyakazi kadhaa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina UNRWA walihusika katika mashambulizi ya Oktoba 7, yaliyofanywa na kudhi la Hamas dhidi ya Israel.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amezisihi serikali kuendelea kutoa ufadhili baada ya mataifa tisa kutangaza kusitisha misaada kwa shirika hilo la Umoja wa mataifa linalowahudumia wakimbizi wa Palestina.
Soma pia: Mahakama ya UN yaitaka Israel kuepusha mauaji ya kimbari Gaza
Mataifa hayo ni Uingereza, Ujerumani, Italia, Uholanzi, Uswisi na Finlanda ambayo yaliungana na Marekani Australia na Canada kusitisha ufadhili huo ambao ni chanzo muhimu cha msaada kwa watu wa Gaza.
Wakati huo huo Wizara ya Afya ya Gaza imesema Jumapili kuwa idadi ya Wapalestina waliouwawa tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na Hamas imefikia watu 26,422. Taarifa ya wizara hiyo imeongeza kuwa takriban watu 165 wameuwawa katika kipindi cha saa 24 zilizopita.