1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Mashambulizi ya kikabila yasababisha maafa Darfur

12 Septemba 2023

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk amesema kuwa mashambulizi yaliyochochewa kikabila na vikosi vya msaada wa dharura RSF yamesababisha vifo vya mamia ya watu katika eneo la Darfur Magharibi.

https://p.dw.com/p/4WFvo
Mkuu wa shirika la haki za binadamu Umoja wa mataifa Volker Turk
Mkuu wa shirika la haki za binadamu Umoja wa mataifa Volker TurkPicha: Pierre Albouy/KEYSTONE/picture alliance

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk amesema kuwa mashambulizi yaliyochochewa kikabila na vikosi vya msaada wa dharura RSF yamesababisha vifo vya mamia ya watu katika eneo la Darfur Magharibi.

Soma pia:

Turk ameliambia baraza la haki za kibinadamu mjini Geneva kuwa, mashambulizi ya kikabila yanayofanywa na RSF na wanamgambo washirika wa Kiarabu yamesababisha vifo vya mamia ya watu hasa wa jamii ya kabila la Masalit.

Mkuu huyo wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kinachoendelea nchini Sudan kinafanana na matukio ya miaka ya nyuma na kamwe vita hivyo havipaswi kuendelea.