UN: Uhaba wa maji watishia mzozo wa kimataifa
22 Machi 2023Matangazo
Tahadhari hiyo imetolewa na Umoja wa Mataifa usiku wa kuamkia leo ambayo ni Siku ya Maji Ulimwenguni.
Richard Connor, mhariri mkuu wa ripoti hiyo amesema asilimia 10 ya watu wote ulimwenguni wanaishi katika maeneo yanayokabiliwa na uhaba mkubwa wa maji.
Kulingana na ripoti hiyo ya Jukwaa la Maji la Umoja wa Mataifa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, asilimia 46 ya watu ulimwenguni kote hukosa huduma za uhakika za usafi.
Ripoti hiyo imetolewa siku moja kabla ya mkutano wa kwanza katika miaka 45 kuhusu maji, ambao umeandaliwa na Umoja wa Mataifa, mjini New York.