1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

UN: Vita vya Ukraine vimesababisha ukiukwaji wa haki

1 Aprili 2023

Kamishna Mkuu wa Ofisi ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa, Volker Turk, ameonya kuwa vita vya Urusi nchini Ukraine vimesababisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu

https://p.dw.com/p/4PaI9
Ukraine-Krieg I
Picha: Russian Defense Ministry Press Service/AP/dpa/picture alliance

Kamishna Mkuu wa Ofisi ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa, Volker Turk, ameonya kuwa vita vya Urusi nchini Ukraine vimesababisha ukiukwaji mkubwa wa haki na kuwavuruga binaadamu kupambana na vitisho vilivyopo dhidi ya maisha yao. Akizungumza mbele ya Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa, Turk alishutumu ukiukwaji wa kutisha uliotendeka tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine miezi 13 iliyopita, na kuonya kuwa mzozo huo unaendelea kusababisha wimbi la mshtuko duniani kote. Turk alidokeza jinsi ongezeko kubwa la bei ya vyakula, nishati na bidhaa nyingine kulivyozidisha hali ya wasiwasi na ukosefu wa usawa kila eneo. Aidha Kamishna huyo alisema ofisi yake imethibitisha vifo vya raia zaidi ya 8,400 na wengine zaidi ya 14,000 kujeruhiwa nchini Ukraine tangu uvamizi wa Urusi ulipoanza.