UN yaelezea hofu juu ya vurugu katika kanda ya Sahel
1 Aprili 2022Matangazo
Katika taarifa jana, MINUSMA imesema hali ya usalama katika eneo la mpaka kati ya Mali, Niger na Burkina Faso, imezorota sana katika wiki za karibuni.
Eneo hilo la mpakani ni eneo lisilo na sheria, na kame ambapo mipaka ya Burkina Faso, Niger na Mali hukutana.
Eno hilo limekumbwa na ghasia tangu mwaka 2015, wakati wapiganaji kaskazini mwa Mali walipojipanga upya baada ya kusambaratishwa na uingiliaji wa kijeshi wa Ufaransa, na kuendeleza kampeni yao katika nchi jirani.
Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa zilizochapishwa Machi 24, karibu raia 600 walikufa nchini Mali mwaka jana, hasa katika matukio yanayohusishwa na wapiganaji wa siasa kali, lakini pia mikononi mwa wanamgambo wa kujilinda na vikosi vya jeshi.