SiasaUingereza
UN yaitaka Uingereza kufirikia upya sheria yake ya uhamiaji
23 Aprili 2024Matangazo
Mkuu wa shirika la Wakimbizi la UNHCR Fillipo Grandi na Kamishina Mkuu wa haki za binadamu Volker Turk, wamesema kuwa muswada wa sheria hiyo uliopitishwa jana usiku, kwa kiasi kikubwa unazuia uwezekano wowote wa kukataa kupelekwa wakimbizi Rwanda hata kama wahamiaji hao watakabiliwa na hatari wakati wa mchakato huo.
Aidha, pia wameeleza kuwa hali za watu huenda zisitiliwe maanani kabla ya kupelekwa Rwanda, kinyume na sheria ya kimataifa ya haki za binadamu.