1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yaondoa wafanyakazi wake kwa uvumi wa kichawi Malawi

Caro Robi
10 Oktoba 2017

Umoja wa Mataifa umesema umewaondoa wafanyakazi wake katika wilaya mbili kusini mwa Malawi ambako taarifa za kuweko kwa 'watu wanaonyonya damu' zimesababisha machafuko na watu wapatao watano kuuwawa.

https://p.dw.com/p/2laP3
Burg Frankenstein bei Darmstadt
Picha: picture-alliance/dpa

Imani za kichawi zimezagaa maeneo ya vijijini nchini Malawi, moja wapo ya nchi masikini kabisa duniani ambako mashirika mengi ya misaada na yasiyokuwa ya kiserikali yana shughuli zao.

Uvumi wa kuweko watu wanaonyonya damu au muumiani uliibuka pia Malawi mwaka 2002.

Idara ya Umoja wa mataifa inayohusika na usalama imesema katika ripoti yake kuhusu usalama katika wilaya za Phalombe na Mulanje kwamba wilaya hizo zimeathirika vibaya na taarifa za kufyonzwa damu kuashiria uwezekano wa kuwepo na Mumiani.

Kutokana na hali hiyo kaimu mratibu mkaazi wa Umoja wa Mataifa Florence Rolle amesema  katika barua pepe iliojibu  maswali kuhusu ripoti kwamba wafanyakazi wa Umoja wa mataifa  wameondoka na kuhamia sehemu nyengine, wakati wengine wangali bado katika Wilaya hizo, ikitegemea ni mahala gani wanafanya shughuli zao.