UN yaonya watu laki nane wapo katika hatari Sudan
20 Aprili 2024Matangazo
Mkuu wa masuala ya kisiasa wa Umoja wa Mataifa Rosemary DiCarlo ameliambia Baraza la Usalama kwamba, mapigano kati ya wanamgambo wa RSF na jeshi la Sudan yanakaribia mji mkuu wa jimbo la Darful wa El Fasher.
Umoja huo umoengeza kuwa karibu watu milioni 25, ikiwa ni takriban nusu ya wakaazi wa Sudan wanahitaji msaada wa kibinadamu huku wengine milioni 8 wakiyakimbia makaazi yao.
Mashirika ya kiraia na Umoja wa Mataifa mwishoni mwa mwezi uliopita, yalisema hatua za haraka zinahitajika ili "kuzuia kuongezeka kwa vifo" kutokana na njaa.
Soma pia:Euro bilioni mbili zapatikana kwa ajili ya kuisaidia Sudan
Siku ya Jumatatu wafadhili waliahidi zaidi ya dola bilioni 2 kwa ajili ya Sudan iliokubwa na vita kwa mwaka mmoja sasa.