1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Zaidi ya watu 600 wafa kwa kimbunga Idai

23 Machi 2019

Idadi ya watu waliokufa kutokana na kimbunga Idai nchini Msumbiji, Zimbabwe na Malawi imeongezeka na kufikia watu 615.

https://p.dw.com/p/3FYna
Mosambik Zyklon Idai | Zerstörung und Hilfe
Picha: Reuters/S. Sibeko

Taarifa hizo zimetolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la uratibu wa misaada ya kiutu, OCHA. Msemaji wa OCHA, amesema watu 417 wamekufa nchini Msumbiji,139 Zimbabwe na 59 Malawi.

Hata hivyo, idadi ya watu waliothibitishwa kufariki inaweza ikaongezeka, kwani bado wanaendelea kupokea taarifa kutoka kwenye maeneo yaliyokumbwa na kimbunga hicho kibaya kilichosababisha mafuriko.

Shughuli za kutoa misaada zinatarajiwa kuendelea kwa kasi, baada ya Umoja wa Mataifa kuongeza kiwango cha msaada wa dharura kutokana na janga hilo na limeonya kuhusu kuenea kwa magonjwa.

Nchi hizo tatu za Kusini mashariki mwa Africa zimewekwa kwenye kiwango cha nchi zinazohitaji msaada wa dharura sawa na Yemen, Sudan na Syria.