1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNICEF: Karibu watoto milioni 400 wananyanyasika majumbani

11 Juni 2024

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), limesema makadirio ya watoto milioni 400 walio chini ya umri wa miaka mitano wanakabiliwa na manyanyaso majumbani.

https://p.dw.com/p/4gt5w
Iraq Mosul | Migogoro | Kufunguliwa upya kwa shule
Watoto wa Mosul wakirejea shuleni huko Iraq.Picha: Maciej Moskwa/NurPhoto/picture alliance

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), limesema makadirio ya watoto milioni 400 walio chini ya umri wa miaka mitano, ikiwa sawa asilimia 60 ya wototo wote wa umri huo duniani kote wanakabiliwa na adhabu ya kipigo au kisaikolojia majumbani mwao, zikiwemo kuchapwa viboko hadi kutukanwa. Makadirio mapya ya UNICEF yanaonyesha data kutoka katika nchi 100 zilizokusanywa kuanzia  2010 hadi 2023, na inashughulikia adhabu ya kimwili na za kisaikolojia. Kwa UNICEF, unyanyasaji wa kisaikolojia unaweza kujumuisha kumzomea mtoto, au kumwita "mpumbavu" au "mvivu," wakati unyanyasaji wa kimwili ni pamoja na kumtikisa, kumpiga au hatua yoyote inayokusudiwa kusababisha maumivu ya kimwili au usumbufu hata pasipo kumsababishia maumivu.Kwa mujibu wa UNICEF zaidi ya mama mmoja au mlezi anayewajibika kwa mtoto kati ya wanne anaamini kwamba adhabu za kimwili ni muhimu ili kuwasomesha ipasavyo watoto wao.