Watoto milioni 67 walikosa chanjo kwa sababu ya UVIKO-19
20 Aprili 2023Matangazo
Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia watoto - UNICEF imesema mafanikio yaliyopatikana kwa taabu katika zaidi ya muongo mmoja katika utoaji chanjo za kawaida kwa watoto yameondolewa.
UNICEF imeelezea wasiwasi wa kuzuka miripuko ya ugonjwa wa kupooza - polio na surua. Utoaji chanjo kwa watoto ulipungua katika nchi 112 na asilimia ya watoto waliopewa chanjo kote ulimwenguni ilishuka kwa pointi tano hadi asilimia 81, ikiwa ni idadi ya chini mno ambayo haijawahi kushuhudiwa tangu mwaka wa 2008. Afrika na Kusini mwa Asia ndio maeneo yaliyoathirika zaidi.