SiasaChina
UN: Tuna wasiwasi baada ya China kuwafunga jela wanaharakati
11 Aprili 2023Matangazo
Xu Zhiyong na mwenzake Ding Jiaxi wote wakiwa ni viongozi wa vuguvugu la kundi la kutetea haki za kiraia lililotaka mageuzi ya katiba na kukosoa ufisadi wa serikali, walipatikana na hatia ya kile kilichotajwa kupindua mamlaka ya serikali katika mashauri yalioendeshwa faraghani.
Turk amesema, wamehukumiwa vifungo virefu, kinyume na sheria za kimataifa za haki za binadamu na kutaka uchunguzi sahihi katika madai yoyote yanayohusu watetezi wa haki za binadamu.
Xu, ambaye alimtaka Rais Xi Jinping ajiuzulu kutokana na jinsi alivyoshughulikia janga la Corona, alifungwa jela miaka 14, huku Ding akifungwa miaka 12 na kunyimwa haki ya kisiasa kwa miaka 3.