Uongozi wa Muungano wa Kenya Moja-OKA unaovijumuisha vyama vinne nchini Kenya umesema kuwa utakuwa na mgombea mmoja wa urais kwenye uchaguzi mkuu ujao mwaka 2022. Hata hivyo Uongozi wa Muungano huo ulikosa kumtaja kiongozi ambaye atakayepeperusha bendera ya muungano huo ukishikilia, kuwa utafanya hivyo wakati mwafaka.