1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani Kongo wauonya utawala kuhusu mageuzi ya katiba

Saleh Mwanamilongo
26 Oktoba 2024

Martin Fayulu amewaambia waandishi wa habari mjini Kinshasa kwamba hakutakuwa na mageuzi au mabadiliko ya yoyote ya Katiba kabla ya uchaguzi mkuu wa 2028.

https://p.dw.com/p/4mGGz
Rais wa Kongo Felix Tshisekedi atangaza mipango ya kuandaa katiba mpya ,akisema ya ilioko sasa inapitwa na wakati
Rais wa Kongo Felix Tshisekedi atangaza mipango ya kuandaa katiba mpya ,akisema ya ilioko sasa inapitwa na wakatiPicha: picture-alliance/AP Photo/J. Delay

Martin Fayulu, ambaye alikuwa kwenye nafasi ya tatu katika uchaguzi wa mwaka jana, amesema Katiba ya sasa haimzuii mtu yeyote kufanya kazi. Kiongozi huyo wa upinzani ametoa wito kwa raia wa Kongo kuwa tayari kuzuia jaribio lolote la magaeuzi ya katiba.

Akiwa ziarani mjini Kisangani, Kaskazini-Mashariki mwa Kongo, Rais Felix  Tshisekedi aliahidi kuteua mwakani, tume ya kitaifa kwa jali ya kuandaa katiba mpya. Tshisekedi amesema katika ya hihi sasa inapitwa na wakati.

Hatua hiyo imeibua wasiwasi miongoni mwa wapinzani, wakimshutumu kutaka kubakia madarakani. Katiba ya sasa ya Kongo ni ya sita tangu nchi hiyo ilipopata uhuru wake kutoka kwa mkoloni Ubelgiji mnamo 1960.

Mwanaharakati wa haki za binadamu na kiongozi wa shirika la The Struggle for Change (LUCHA) linalotetea haki za kijamii Fred Bauma amesema Tshisekedi anaendelea kukaidi katiba wakati aliapa kuilinda na kuitetea wakati alipoapishwa mapema mwaka huu.