Wapinzani wataka kumg'oa kaimu Rais wa Korea Kusini
27 Desemba 2024Kaimu Rais wa Korea Kusini, Han Duck-soo, anakabiliwa na kura ya kumwondoa madarakani leo Ijumaa huku mzozo wa kisiasa ukizidi, baada ya Rais Yoon Suk Yeol kusimamishwa kufuati tangazo lake la sheria ya kijeshi mnamo Desemba 3.
Wabunge wa upinzani wanamtuhumu Han kwa kukwamisha mchakato wa kumwondoa Yoon kwa kukataa kuidhinisha majaji watatu wa Mahakama ya Katiba, ambao ni muhimu kwa uamuzi wa hatma ya Yoon.
Soma pia: Rais wa Korea Kusini aondolewa madarakani na Bunge
Iwapo atang'olewa, Waziri wa Fedha Choi Sang-mok atachukua nafasi yake, hatua ambayo itakuwa ya kwanza katika historia ya Korea Kusini kumwondoa kaimu rais, na itazidi kuyumbisha hali ya kisiasa.
Han anasisitiza kuwa ataidhinisha majaji hao endapo vyama vyote viwili vitafikia mwafaka kuhusu uteuzi wao.