1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Upinzani Korea Kusini yakumuondoa kaimu rais

26 Desemba 2024

Upinzani nchini Korea Kusini umesema umewasilisha mswada wa kumuondoa madarakani kaimu rais Han Duck-soo. Hatua hiyo inauendeleza mzozo kuhusu muundo wa Mahakama ya Kikatiba ambayo itaamua hatima ya mtangulizi wake.

https://p.dw.com/p/4oaSG
Waziri Mkuu wa Korea Kusini Han Duck-soo
Waziri Mkuu Han Duck-soo alichukua usukani kuwa kaimu rais baada ya Yoon Suk Yeoul kuvuliwa madaraka na bungePicha: Yonhap AP/picture alliance

Korea Kusini ilitumbukia katika mgogoro wa kisiaa wakati Rais Yoon Suk Yeol, ambaye ameachishwa kazi kwa sasa, alitangaza amri ya kijeshi Desemba 3. Yoon alivuliwa majukumu yake na bunde Desemba 14, lakini uamuzi wa mahakama ya kikatiba unaounga mkono kura ya kutokuwa na imani na wabunge unahitajika ili kukamilisha mchakato huo.

Soma pia: Korea Kusini: Aliyekuwa Rais akaidi agizo la kuhojiwa

Mahakama hiyo hata hivyo ina upungufu wa majaji watatu. Hata kama inaweza kuendelea na mchakato huo na majaji wake sita, kura moja ya kupinga inatosha kumrejesha ofisini Yoon. Upinzani unamtaka rais wa sasa Han aidhinishe majina ya majaji watatu walioteuliwa, jambo ambalo amekataa kulifanya mpaka sasa, na kuacha pande zote mbili kwenye mkwamo.

Kwa hivyo Chama cha upinzani cha Democratic kinataka kaimu rais huyo naye ashtakiwe na kuondolewa madarakani.