1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Upinzani wa Uturuki kutumia waangalizi 500,000 uchaguzi ujao

29 Aprili 2023

Kambi kuu ya upinzani nchini Uturuki inapanga kuwatawanya karibu waangalizi 500,000 kufuatilia matokeo ya uchaguzi wa Mei 14 huku kukiwa na wasiwasi wa kufanyika vitendo vya kilaghai

https://p.dw.com/p/4QiNh
Türkei, Ankara | Oppositionsbündnis nominiert Kemal Kılıçdaroğlu als Präsidentschaftskandidat
Picha: Alp Eren Kaya/Republican People's Party/Handout/REUTERS

Hayo yamesemwa na kundi hilo lenye kuongozwa na chama kiitwacho-Republican People's Party (CHP). Akizungumza na waandishi wa habari msimamizi wa jitihada za usalama katika uchaguzi wa muungano huo, Oguz Kaan Salici amesema idadi hiyo ya watu itapelekwa katika vituo 50,000 vya kupigia kura, ikijumusha masanduku 192,000 nchini kote.

Soma zaidi:Uturuki: Vyama vya upinzani kusimama pamoja dhidi ya Erdogan katika uchaguzi wa Mei 14

Muungano huo wenye kujumuisha vyama sita ulisema kuna wasiwasi mkubwa juu ya usalama wa uchaguzi, ikiwa ni pamoja na matatizo ya kiufundi yanayoweza kutokea wakati wa kupiga kura au siku ya kuhesabu kura hizo.

Katika chaguzi zilizopita, ikiwemo ya 2019, shirika la habari la Uturuki-Anadolu lilifikwa na wakati mgumu baada ya kudaiwa kufanya udukuzi wa takwimu. Umoja huo unapanga kutoka takwimu zake kutoka katika vituo vya kuhesabu kura.