Amama Mbabazi na Kizza Besigye wanasema Tume Huru ya Uchaguzi kwa kushirikiana na chama tawala cha NRM wanafanya njama ya kutoa matokeo yasiyokuwa sahihi ya uchaguzi wa Februari 18 na ndio sababu wanawazuwia mawakala wao kuwa na simu za mkononi vituoni.